• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 30, 2012

  KAPTENI GADNA G ATUA MASKANI LA TIMES FM 100.5

  Gadna akizungumza na Waandishi wa Habari katika mgahawa wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji leo. Wengine kulia kwake ni Scholastica Mazula, Cliffor Ndimbo na Hadija Shaibu 'Dida'. Kulia ni Jabir Saleh. Watangazaji wa Times Radio 100.5. FM

  Gadna kushoto akiwa na Schola na mtangazaji mwingoine mpya wa Times, Natasha ambaye anatangaza kipindi cha Filamonata.

  William Malacela akimpongeza Gadna

  Waandishi wa Habari waliohudhuria utambulisho wa Gadna Times FM leo wakipata maakuli 

  MTANGAZAJI Super Star bongo, Gadna G. Habash leo ametambulishwa rasmi kuhamia Radio Times FM, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili, tangu aipige chini Clouds FM.
  Sauti tamu ya mume huyo wa mwanamuziki nyota Tanzania, Lady Jaydee sasa itakuwa ikisikika kwenye kipindi cha Maskani, kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa1:00 usiku.
  Mara ya mwisho, Kapteni G alikuwa akitangaza kipindi cha Jahazi Clouds kabla ya kubwaga manyanga Novemba mwaka 2010 katika kipindi ambacho redio hiyo ilipoteza mastaa wengi, wakiwemo Fina Mango, George Njogopa na Masoud Kipanya.   
  Fina kwa sasa yupo Magic FM na Kipanya alimtangulia Gadna Times. Kwa sasa, bila kutafuna maneno, Times FM ipo juu ‘kinoma’ katika FM radio za kibongo na nyingine nyingi zimebakiza umaarufu wa majina tu.
  Mona na mama yake, watangazaji wa Filamonata Times FM

  Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto katikati, kulia Mkurugenzi wa Jambo Concept Inc, Benny Kisaka na William Malecela, walikuwepo kwenye utambulisho huo 

  Willy Malecela akiwa na vifaa vya Times FM

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAPTENI GADNA G ATUA MASKANI LA TIMES FM 100.5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top