• HABARI MPYA

    Tuesday, August 21, 2012

    RAIS KIKWETE AWAITA YANGA IKULU, MANJI, MAMA KARUME WAENDA KUFUNGUA TAWI RWANDA

    Kikosi cha Yanga na Kombe la Kagame

    Na Prince Akbar
    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakata Mrisho Kikwete amewapa mwaliko mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati mara mbili mfululizo, Yanga SC kupeleka Kombe lao Ikulu.
    Rais Kikwete
    Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji amesema kwamba wanashukuru kwa mwaliko huo na watakwenda huko, wakirejea kutoka Rwanda ambako kikosi chao kinakwenda jioni hii.
    Manji pia alisema wanatarajia kufungua tawi la klabu yao nchini Rwanda, kufuatia uhusiano mzuri uliopo, baina ya klabu hiyo na nchi hiyo kwa pamoja na rais wake, Paul Kagame.
    Manji alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ta Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kuhusu mwaliko wa mabingwa hao Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kutoka kwa rais wa Rwanda, Kagame.
    Manji akizungumza na wachezaji wa Yanga
    “Tunategemea kufungua tawi jipya la Yanga nchini Rwanda, hiyo itasaidia kuongeza wanachama nje ya nchi kwa kuanzia na Rwanda,”alisema Ofisa huyo Mtendaji Mkuu wa Quality Group Limited.
    Yanga itakua Rwanda kwa wiki moja kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wakiwa watacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Rayon Sports, Polisi na APR.
    Kuhusu mchezaji mpya aliyesajiliwa kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na APR ya Rwanda, Mbuyu Twite, Manji alisema  ataungana na wenzake nchini Rwanda na mara baada ya kambi hiyo ya wiki moja atarudi na timu kuja kuanza kuitumikia katika msimu mpya w aligi kuu.
    Yanga inakwenda Rwanda na msafara wa watu 42, wakiwemo wachezaji 29, Maofisa watano wa benchi la Ufundi na viongozi wanane.
    Viongozi wanaondoka na timu ni Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini Mama Fatma Karume, Francis Kifukwe na Seif Ahmed ‘Magari’ sambamba na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Abdallah Bin-Kleb na Salum Rupia.
    Benchi la ufundi ni kocha mkuu; Tom Saintfiet, Kocha Msaidizi Fred Felix Minziro, Meneja Hafidh Saleh, Daktari, Sufiani Juma na Mtunza vifaa Mahmoud Omary ‘Mpogolo’, wakati wachezaji ni makipa: Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Said Mohamed. Mabeki Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, Stefano Mwasyika, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Ibrahim Job, Ladisalus Mbogo; viungo Athumani Iddi ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Simon Msuva, Shamte Ally, Omega Seme, Idrisa Rashid, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Nurdin Bakari na washambuliaji; Said Bahanunzi ‘Spider Man’, Hamis Kiiza ‘Diego’, Jerry Tegete na Didier Kavumbangu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS KIKWETE AWAITA YANGA IKULU, MANJI, MAMA KARUME WAENDA KUFUNGUA TAWI RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top