• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 24, 2012

  TAIFA STARS YAUA TAIFA CUP

  Taifa Stars

  Na Prince Akbar
  MICHUANO ya Kombe la Taifa (Taifa Cup) inayoshirikisha kombaini za mikoa ya Tanzania Bara haitakuwepo mwaka huu kutokana na kukosekana kwa udhamini.
  Taarifa ya TFF imesema licha ya kukosekana kwa udhamini, awali walifikiria kuendesha mashindano hayo kwa michango ya wanachama wetu (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) na Serikali za mikoa kugharamia timu zao.
  Lakini baadhi ya wanachama wetu na Serikali za mikoa walishauri kuwa ni ngumu kuendesha mashindano hayo kwa sasa kutokana na shughuli za kitaifa zinazoendelea hivi sasa ikiwemo maandalizi ya sensa ya watu na makazi.
  Kwa mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mashindano ya Kombe la Taifa yalitakiwa kufanyika kuanzia Julai 23 hadi Agosti 6 mwaka huu.
  Michuano ya Kombe la Taifa msimu uliopita ilidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao sasa ni wadhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars na Mbeya waliibuka mabingwa katika fainali iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
  Wakati TBL wanadhamini Taifa Cup, kampuni nyingine ya bia nchini, Serengeti (SBL) ndio walikuwa wadhamini wa Taifa Stars.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAUA TAIFA CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top