Sir Alex Ferguson anatarajia mambo makubwa kwa kinda, Danny Welbeck baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka minne na Manchester United.
Kinda huyo wa umri wa miaka 21, amefunga mabao 17 tangu aanze kuichezea timu hiyo miaka minne iliyopita na kufanikiwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza na bosi huyo wa Old Trafford anatarajiwa makubwa zaidi kuanzia sasa.
Danny Welbeck akisaini mkataba mpya na Mtendaji Mkuu wa Manchester United, David Gill
"Danny amekuwa kwenye timu tangu ana miaka nane na amefanya vizuri kwa miaka kadhaa iliyopita – wa kwanza akicheza kwa mkopo (Sundeland) na wa pili mwaka jana kama mchezaji wa kikosi cha kwanza,'alisema Ferguson.
Welbeck anakabiliwa na ushindani wa kugombea namba sasa baada ya kusajiliwa Robin van Persie
Welbeck amecheza mechi 30 za Ligi Kuu msimu uliopita mbele ya washambuliaji wanaomzidi umri na uzoefu aliokuwa akishindania nao namba Old Trafford— Dimitar Berbatov, Javier Hernandez na Michael Owen aliyeondoka.
Alifunga mabao tisa katika ligi United kabla ya kuchukuliwa kwenye kikosi cha Euro 2012 na kocha mpya wa England, Roy Hodgson. Msimu huu, Ferguson anatarajia mabao yasiyopungua 20 kutoka Welbeck, ambaye sasa amekwishaichezea England mechi tisa.
Welbeck alikuwa mchezaji wa uhakika katika kikosi cha kwanza cha United msimu uliopita baada ya kucheza kwa mkopo Sunderland
Anatakiwa kuwa katika kiwano kizuri, baada ya kusajiliwa kwa Robin van Persie kwa pauni Milioni 24 kutoka Arsenal.
Katika mkataba wake mpya, imeripotiwa atakuwa analipwa pauni 75,000 kwa wiki.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk


.png)
0 comments:
Post a Comment