• HABARI MPYA

    Tuesday, August 21, 2012

    ARSENAL WAMWAGA VIFAA AIRTEL RISING STAR

    Mkrugenzi wa Masoko wa Arsenal, Angus Kinnear akimkabidhi jezi, Waziri Mkuu wa  Kenya, Raila Odinga (kushoto) katika sherehe za uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Africa mjini Nairobi leo.

    Nairobi, Kenya
    MICHUANO ya Airtel Rising Stars barani Afrika imetimua vumbi   Jijini Nairobi, Kenya. Michuano hiyo imeleta pamoja wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba na itaendelea mpaka Agosti 25.
    Michuano hiyo ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa na kufanyika kwenye nchi 15 barani Afrika. Huu ni mpango kabambe wa Airtel Rising Stars, wenye lengo la kuwapa vijana chipukizi fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Ikiwa ni ya moja ya michuano mikubwa kabisa barani Afrika, jumla ya timu 18,000 zilishiriki na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana kushiriki. Hii ndio mara ya kwanza kushirikisha wasichana.
    Michuano hiyo ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Kenya, Mh Raila Odinga – akisindikizwa na Mtendaji Mkuu wa Bharti Airtel Afrika – Manoj Kohli
    Michuano hiyo pia itaashiria uzinduzi wa kliniki mbili za soka za kimataifa zitakaozoendezwa na makocha kutoka klabu kubwa duniani – Arsenal na Manchester United – zote za Uingereza. Kwenye uzinduzi wa michuano hiyo pia walikuwa waakilishi kutoka kwenye Klabu hizo – Mkurugenzi wa Masoko kutoka Manchester United Jonathan Rigby na Mkurugenzi Masoko kutoka Arsenal Angus Kinnear. Uzinduzi wa kliniki utafanyika na wachezaji wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel na Ray Parlour kutoka Arsenal.
    Kwenye mechi za ufunguzi, timu ya wasichana ya Kenya ilishushia kipigo cha magoli 11 wenzao wa Malawi wakati kwa upande wa wavulana Malawi ilishinda 5- dhidi ya Kenya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL WAMWAGA VIFAA AIRTEL RISING STAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top