• HABARI MPYA

    Tuesday, August 28, 2012

    SIMBA SC: TFF KAMA WANATUHUJUMU HIVI USAJILI WA OCHIENG


    Hans Poppe kushoto akimkabidhi jezi Ochieng kulia. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'
    Na Mahmoud Zubeiry 
    MABINGWA wa soka Tanzania, Simba SC imesema inahisi dalili za kutotendewa haki katika usajili wake kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Kwa nini? Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba klabu yake imekwishakamilisha usajili wa beki Paschal Ochieng kutoka AFC Leopard ya Kenya, lakini ajabu TFF inashindwa kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kwa mujibu wa taratibu.
    “Baada ya sisi kumalizana na klabu na mchezaji, TFF wanatakiwa kutuma maombi ya ITC (Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) katika mfumo wa mtandao, kila tukiwapigia simu viongozi wa FKF (Shirikisho la Soka Kenya) wanasema wanasubiri maombi kutoka TFF na bado hayajatumwa, kwa kweli hii inasikitisha sana na tunahisi kuna dalili za kutotendewa haki,”alisema Hans Poppe. BIN ZUBEIRY ilijaribu kuwasiliana nja Ofisa anayehusika na masuala ya uhamisho wa kimataifa TFF, Sadi Kawemba, lakini kwa bahati mbaya hakuwa karibu na simu yake, licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu. Awali, kulikuwa kuna malalamiko kutoka AFC Leopard juu ya usajili wa Ochieng, lakini Simba ikafanikiwa kumaliza utata huo kwa kuilipa klabu yake. Ochieng ni miongoni mwa wachezaji watano wa kigeni watakaokuwamo kwenye kikosi cha Simba cha msimu ujao, wengine wakiwa ni kiungo Komabil Keita, washambuliaji Felix Sunzu kutoka Zambia, Emmanuel Okwi kutoka Uganda na Daniel Akuffo kutoka Ghana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC: TFF KAMA WANATUHUJUMU HIVI USAJILI WA OCHIENG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top