• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 29, 2012

  NI BARCA TENA AU REAL SUPER CUP HISPANIA?

  Kushoto Mourinho, akifuatiwa na Pepe na mbele ni Modric mazoezini juzi Bernabeu. Mechi hiyo itaanza saa 5:30 usiku leo

  Carles Puyol 

  NAHODHA wa Barcelona, Carles Puyol anaweza kucheza mechi ya marudiano ya Super Cup ya Hispania leo dhidi ya Real Madrid licha ya kuumia na kocha Tito Vilanova amesema itabidi mask kujilinda.

  Beki wa kati, Puyol, ambaye aliumia Jumapili Barca ikishinda 2-1 katika La Liga dhidi ya Osasuna, alifanya mazoezi na wenzake jana na Vilanova amesema anaweza kumpanga leo.
  "Kama madaktari watasema ni hatari kumtumia, hatacheza. Hatuwezi kumhatarisha Carles kwa vyovyote."
  Barca pia itamkosa kiungo Ibrahim Afellay ambaye alifanyiwa upsuaji wa goti Oktoba, ingawa amepona na alikuwepo kwenye kikosi cha Uholanzi katika Euro 2012.
  Vyombo vya Habari Hispania tayari vinamhusisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na kuhamia Liverpool ya England au klabu nyingine ya Serie A.

  Kocha Jose Mourinho amepania kushinda mechi hiyo ili kuhakikisha Real Madrid imezinduka baada ya kufungwa Getafe katika La Liga.
  Wanatakiwa kukipiku kipigo cha mabao 3-2 walichofungwa kwenye mechi ya kwanza ili kutwaa Super Cup na Mourinho amesema anataka kuona mabadiliko makubwa ya kiuchezaji leo.
  Katika mchezo wa leo, Real inaweza kumtumia kiungo wake mpya, Luka Modric iliyekamilisha usajili wake juzi kutoka Tottenham Hotspur.
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia alifanya mazoezi na wachezaji wenzake juzi jioni na Mourinho amesema anaweza kuwa tayari kucheza.
  Beki wa kati, Pepe, ambaye aliumia kichwa katika sare ya 1-1 nyumbani na Valencia katika mechi ya ufunguzi yaLa Liga, alifanya mazoezi ya kawaida juzi na anaweza kuanza leo.
  Kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita, Barca imeshinda Super Cup, inayokutanisha bingwa wa Kombe la Mfalme na bingwa wa Ligi Kuu na mara ya mwisho Real ilitwaa taji hilo mwaka 2008.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI BARCA TENA AU REAL SUPER CUP HISPANIA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top