• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 24, 2012

  AZAM FC WAMTMUA BLACKBERRY

  Odhiambo 'Blackberry'

  Na Mahmoud Zubeiry
  AZAM FC imevunja mkataba na kiungo George Odhiambo ‘Blackberry’, baada ya mchezaji huyo wa Kenya kukiuka mkataba wake, kitendo ambacho kimechukuliwa kama ni utovu wa nidhamu, imeelezwa.
  “Blackberry hajaonekana mazoezini siku sita na kwa sababu hiyo, klabu imevunja naye mkataba. Huyu mchezaji kwa kweli ametuangusha sana,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.
  Pamoja na kusajiliwa kwa matumaini makubwa, kiungo huyo bora wa zamani wa Ligi ya Kenya, alishindwa mapema tu kudhihirisha uwezo wake katika soka ya Tanzania, kuanzia kwenye Kombe la Urafiki na baadaye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
  Kwa kuondolewa Blackberry, Azam sasa inabaki na wachezaji wanne wa kigeni, ambao ni mabeki Ibrahim Shikanda kutoka Kenya, Joseph Owino kutoka Uganda na viungo Kipre Michael Balou na Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory Coast.
  Kuna uwezekano Azam ikasajili mshambuliaji mwingine kutoka Ivory Coast, kuziba nafasi ya Odhiambo.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAMTMUA BLACKBERRY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top