• HABARI MPYA

    Saturday, August 25, 2012

    TBL YAMWAGA VIFAA LIGI KUU ZANZIBAR

    Mh Machano Othman Said, Waziri Asiye na Wizara Maalum Zanzibar (kushoto) akizungumza na viongozi wa klabu za Ligi Kuu ya soka ya Grand Malt Zanzibar, kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zote 12 zitakazoshiriki ligi hiyo. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL, watengenezaji wa Grand Malt), Fimbo Buttalah.



    Mh Machano Othman Said akimkabidhi vifaa mwakilishi wa Jamhuri ya Pemba, kulia ni Fimbo Bittala na Makamu wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ally Mohamed.

    Mh Machano akimkabidhi vifaa mwakilishi wa Falcon ya Pemba, kulia ni Fimbo na Ally Mohamed. Falcon na Jamhuri zitapambana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi ya Septemba 1, usiku Uwanja wa Amaan.  Picha zote kwa hisani ya Intellectuals Communications Limited
    Na Prince Akbar
    SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeipongeza Grand Malt kwa kudhamini Ligi Kuu, ambapo kwa sasa inaamini itakuwa yenye ushindani mkubwa.
    Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View leo, Waziri Asiye na Wizara Maalum katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Machano Othman Said, alisema huo ni mwanzo mzuri kwa soka la Zanzibar.
    “Huu ni mwanzo mzuri kwa soka la Zanzibar na naamini tutafikia mafanikio yale tuliyokusudia. Nawashukuru Grand Malt kwa hili.
    “Ila ninawaomba wadau wote wa ligi hii kuanzia Grand Malt, ZFA (Chama cha Soka Zanzibar) na klabu viweke wazi mikataba yote ili kusiwe na manung’uniko,” alisema.
    Alizishauri klabu zote kufanya maandalizi mapema ili kuweza kuifanya ligi hiyo iwe ya ushindani mkubwa na kuvitaka kuhakikisha zina timu za vijana ili kuweza kupata timu bora kuanzia chini mpaka ngazi ya taifa.
    Alisema ligi ilikosa msisimko katika miaka ya hivi karibuni kutokana na lkukosa mdhamini na ana uhakika kwa sasa kila kitu kitakuwa sawa.
    Kwa upande wake, Meneja Masoka wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), watengenezaji wa  Grand Malt, Fimbo Butallah alisema wameamua kudhamini ili kuleta changamoto na ushindani katika soka ya Zanzibar, kauli iliyoungwa mkono na Makamu wa Rais wa ZFA, Ally Mohamed. Timu hizo zilikabibidhiwa jezi, mipira, vizuia ugoko pamoja na vifaa vinginevyo.
    Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Super Falcon, Jamhuri , Chipukizi, Duma, Mundu, Mafunzo, KMKM, Mtende, Malindi, Bandari, Zimamoto na Chuoni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TBL YAMWAGA VIFAA LIGI KUU ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top