• HABARI MPYA

    Sunday, August 26, 2012

    AKINA BANKA WAKIMBIZA KWA KASI YA USAIN BOLT KENYA

    David Naftali

    Na Princess Asia
    BANDARI ya Mombasa, Kenya inayopigwa tafu na wachezaji wanne wa Kitanzania, David Naftali, Meshack Abel, Mohamed Banka na Thomas Maurice, imeendelea kujiimarisha katika harakati za kurejea Ligi Kuu ya Kenya, baada ya jana kuifunga mabao 2-0 Moyas ya Nairobi.
    Bandari ilipata bao lake la kwanza dakika ya tano, mfungaji Thom Mouricekwa mpira wa adhabu, kabla ya Erick Okoth kufunga la pili dakika ya 38.
    Kwa ushindi huo, Bandari imefikisha pointi 60, ikizidi kuwaacha mbali wapinzani wao, Kariobang Sharks wenye pointi 49 katika nafasi ya pili, baada ya kutoka sare na Kongo United (JMJ) jana.
    Bandari inatarajiwa kuondoka Mombasa kesho kuja Dar es Salaam kwa ziara ya wiki moja ya kucheza mechi za kujipima nguvu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AKINA BANKA WAKIMBIZA KWA KASI YA USAIN BOLT KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top