• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 31, 2012

  SERENGETI KUJIPIMA NA ASHANTI


  Na Princess Asia 
  TIMU ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys iliyokuwa kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya itavunja rasmi kambi yake kesho kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ashanti United.
  Mechi hiyo dhidi ya Ashanti United iliyoko daraja la kwanza itachezwa kuanzia saa 10 jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 2,000.
  Serengeti Boys ilikuwa Septemba 9 mwaka huu icheze na Kenya kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, lakini Kenya ikajitoa ambapo sasa itacheza na Misri katika raundi ya pili. Mechi ya kwanza itachezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
  Mwishoni mwa Septemba, Serengeti Boys itarejea tena kambini kujiandaa kuikabili Misri ambapo kabla inatarajia kupata mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu itakayotangazwa baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI KUJIPIMA NA ASHANTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top