• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 27, 2012

  RASMI KEITA AMUENGUA MUDDE SIMBA SC

  Mudde kulia

  Na Prince Akbar
  SIMBA imetema kiungo Mganda, Mussa Mudde katika usajili wake, kwa sababu imegundulika, majeruhi yake yatamuweka nje ya Uwanja kwa muda mrefu na badala yake imemsajili beki kutoka Mali, Komabil Keita.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema jioni hii kwamba, Mudde atakuwa nje ya Uwanja kwa miezi mitatu hivyo hataweza kucheza kabisa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na kwa sababu hiyo anaondolewa na nafasi yake anapewa Keita.  
  Tayari Keita yupo na Simba kambini mjini Arusha na ingawa jana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mathare United, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha aliumia na kutoka nje Wekundu wa Msimbazi wakishinda 2-1, lakini imeelezwa leo alifanya mazoezi na wenzake.
  Kwa marekebisho hayo, wachezaji wa kigeni wa Simba SC wanakuwa ni Keita, Emmanuel Okwi kutoka Uganda, Daniel Akuffo kutoka Ghana, Felix Sunzu kutoka Zambia na Paschal Ochieng kutoka Kenya.    
  Aidha, Mudde anakuwa mchezaji wa kigeni wa tatu kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao na kutemwa kabla ya kuanza kazi, wengine wakiwa ni Lino Masombo na Kanu Mbivayanga, wote kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RASMI KEITA AMUENGUA MUDDE SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top