• HABARI MPYA

    Wednesday, August 22, 2012

    SIMBA YAMALIZA UTATA SUALA LA OCHIENG, ITC YAKE YAJA LEO

    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kushoto akimkabidhi jezi Paschal Ochieng baada ya kusaini mkataba na klabu hiyo. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'

    Na Mahmoud Zubeiry
    SIMBA SC imemaliza utata wa usajili wa beki wake wa kimataifa wa Kenya, Paschal Ochieng kutoka AFC Leopard ya Kenya na sasa hakuna shaka atachezea Wekundu hao wa Msimbazi msimu mpya.
    Habari za ndani kutoka Simba SC, zimesema kwamba, Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, chini ya Mwenyekiti wake, Zacharia Hans Poppe ilikutana na klabu hiyo bingwa ya zamani ya Kenya na kumaliza tofauti zao.
    Leopard ilikuwa inadai Simba imemsajili Ochieng kinyume na utaratibu, kwani bado ana mkataba na klabu yake hiyo wa miezi sita.
    Kwa sababu hiyo, Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya beki huyo wa zamani wa Yanga, inatarajiwa kuwasili nchini kuanzia leo.
    Ochieng ni miongoni mwa wachezaji watano wa kigeni watakaokuwamo kwenye kikosi cha Simba cha msimu ujao, wengine wakiwa ni kiungo Mussa Mudde, ambaye hata hivyo inaelezwa anaweza kukatwa akasajiliwa Keita wa Mali, washambuliaji Felix Sunzu kutoka Zambia, Emmanuel Okwi kutoka Uganda na Daniel Akuffo kutoka Ghana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAMALIZA UTATA SUALA LA OCHIENG, ITC YAKE YAJA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top