• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 29, 2012

  TALENT MISS ILALA KESHO KWA JAYDEE


  Vimwana Miss Ilala
  Na Princess Asia
  VIMWANA 14 wanaotarajiwa kupanda jukwaani kuwania umalkia wa Kanda ya Manispaa ya Ilala, Redds Miss Ilala 2012 kesho Agosti kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, watamenyana kuwania taji la mrembo mwenye kipaji, ikiwa ni sehemu ya kuelekea shindano lenyewe litakalofanyika Septemba 7, mwaka huu.
  Warembo hao ambao wamejiandaa vilivyo kila mmoja akiwa amejiandaa katika kipengele anachokimudu zaidi, wamekuwa wakipata maelekezo ya kuboresha wanachotaka kukifanya kwa walimu wa fani ya sanaa mbalimbali.
  Katika shindano hilo litakaloanza saa 2;00 usiku, bendi ya mapacha watatu watatumbuiza ndani ya ukumbi huo kwa kiingilio cha sh 10,000 tu. Redds Miss Ilala inayoshikilia taji la Miss Tanzania kupitia mrembo wake, Salha Israel, tumejiandaa vilivyo mwaka huu kuonesha mambo mengi yatakayowavutia mashabiki siku ya shindano hilo.
  Mbali ya maandalizi ya shoo, pia mwaka huu tumejiandaa vizuri kuhakikisha taji hilo linaendelea kubaki katika manispaa yetu na ili katika kujiweka sawa na hilo, warembo wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya ukufunzi wa Slyvia Mashuda tayari kwa shindano hilo litakalofanyika Septemba 7 kwenye ukumbi wa nje wa Nyumbani Lounge.
  Slyvia ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008, akiwa Miss Ilala wa mwaka huo akishiriana na Neema Mbuya sanjari na Dickson Daudi wa THT katika shoo. Miss Ilala ambayo tumeshatoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe aka K-Lyne), 20029( Angela Damas Mutalimwa) na  Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel anayeshikilia taji hilo.
  Warembo hao kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika Club ya Nyumbani Lounge, iliyopo maeneo ya Namanga, Dar es Salaam. Washiriki hao ni pamoja na  Mary Chizi, Matilda Martin, Magdalena Munisi, Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris na Elizaberth Pertty.
  Warembo wengine ni Wilmina  Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe, Noela Michael na Phillios Lemi.
  Mbali ya Uhuru One, Wadhamini wengine katika mashindano hayo ni pamoja na Dodoma Wine, City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM na Redds Premmium Cold. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TALENT MISS ILALA KESHO KWA JAYDEE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top