• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 31, 2012

  MAWAKALA WAPYA FIFA KUTAHINIWA JUMAMOSI

  Yussuf Bakhresa

  Na Dina Zubeiry
  MTIHANI kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) utafanyika Septemba 27, mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF. Ada ya mtihani ni dola 50 za Marekani.
  Pia Damas Ndumbaro na Ally Mleh wa Manyara Sports Management ambao tayari ni mawakala wanaotambuliwa na FIFA wanatakiwa kufanya mtihani huo kama wanataka kuendelea na uwakala kwa vile muda wa leseni zao za awali umemalizika.
  Mawakala wengine ambao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully leseni zao bado ziko hai.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAWAKALA WAPYA FIFA KUTAHINIWA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top