Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya
CHELSEA KUSAINI BEKI LA NGUVU LA HISPANIA
Beki wa kulia wa Marseille, Cesar Azpilicueta amesema amekuwa akifuatiliwa na Chelsea ili akachukue mikoba Jose Bosingwa. Azpilicueta, aliyezaliwa miaka 22 iliyopita, alikuwemo kwenye kikosi cha Hispania kilichoshiriki Michezo ya Olimpiki mjini London mwaka huu.
Arsenal itatumia mamilioni iliyopata kwa mauzo ya Alex Song kwenda Barcelona kumsajili kiungo mkabaji Cheick Tiote, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Newcastle United.
Rennes ya Ufaransa, inatarajia kiungo wake kinda, Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka 21, ataondoka kwenye klabu hiyo wiki hii. Timu hiyo ya Ligue 1 imesema imepokea ofa Tottenham, Zenit St Petersburg na klabu nyingine ya tatu ambayo hawakuitaja, ambayo hata hivyo inaaminika kuwa ni Arsenal.
Tottenham ipo karibu kumnasa mshambuliaji wa Brazil, Willian, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Shakhtar Donetsk kwa pauni Milioni 20, na pia imefufua nia kumsajili nyota wa Internacional, Leandro Damiao, mwenye umri wa miaka 23 aliyetwaa Medali ya Fedha na Brazil katika Olimpiki ya mwaka huu London.
Sunderland inajiandaa kutumia zaidi ya pauni Milioni 25 katika siku tisa zijazo kwa usajili wa winga wa Manchester City, Adam Johnson mwenye umri wa miaka 25, mshambuliaji wa Wolves, Steven Fletcher, mwenye umri wa miaka 25 nabeki wa Blackburn, Martin Olsson mwenye miaka 24.
Mustakabali wa Robert Green kama kipa namba moja wa QPR unaweza kuwa shakani, baada ya mechi moja tu ya Ligi Kuu kutokana na kocha Mark Hughes kuonyesha dalili za kumsajili kipa wa Celtic, Artur Boruc mwenye umri wa miaka 32, ambaye kwa sasa yuko huru.
Liverpool inaona bora mshambuliaji wake, Andy Carroll mwenye umri wa miaka 23 akae benchi msimu mzima, kuliko kumuuza kwa bei ya chini kwa wapinzani wao katika Ligi Kuu.
Newcastle iliyoonyesha nia ya kumrudisha Carroll, imesema hataongeza dau kutoka pauni Milioni 12 walizoahidi kwa ajili ya mchezaji huyo, ambaye The Magpies walimuuza kwa Wekundu wa Anfield pauni Milioni 35, Januari mwaka jana.
Newcastle na Fulham zinamfuatilia beki wa FC Twente, Douglas. Mzaliwa huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 anacheza chini ya kocha wa zamani wa England, Steve McLaren katika Ligi Kuu ya Uholanzi.
ARTETA AWAASA MASHABIKI
Kiungo wa Arsenal, Mikel Arteta, mwenye umri wa miaka 30, amesema mashabiki wa Gunners wanatakiwa kukipa muda wa kutosha kikosi kipya cha kwanza cha timu hiyo, kabla ya kuwa imara. Habari kamili: Daily Telegraph
ANDERSON
Kiungon wa Manchester United, Mbrazil Anderson mwenye umri wa miaka 24, amechukizwa na kukosewa kwa jina lake katika jezi na kuandikwa 'Andesron' kwenye mechi ambayo Mashetani Wekundu walipigwa 1-0 na Everton Uwanja wa Goodison Park Jumatatu.


.png)
0 comments:
Post a Comment