• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 28, 2012

  SUNZU AFIWA NA DADA YAKE, AENDA MSIBANI DRC

  Felix Sunzu

  Na Princess Asia
  MSHAMBULIAJI Mzambia wa Simba SC, ameondoka nchini leo nchini kuelekea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuhudhuria msiba wa dada yake ambaye alifariki dunia juzi jioni nchini humo.
  Taarifa ya Simba SC, imesema kwamba dada huyo wa mshambuliaji huyo, alikuwa amekwenda kumtembelea ndugu yao, beki Stopila, anayechezea Tout Puissant Mazembe siku sita zilizopita, lakini akakumbwa na umauti kutokana na ugonjwa wa Malaria ulimpanda kichwani (Cerebral Malaria).
  Uongozi wa Simba umetoa pole kwa familia ya Sunzu pamoja na kufanikisha kuondoka kwa haraka kwa mchezaji huyo ili akaungane na familia yake.
  Sunzu atarejea nchini baada ya kumaliza maziko na klabu ya Simba inaomba vyombo vya habari na wadau wengine kumpa nafasi ya kuomboleza msiba huu mzito kwake binafsi, kwa familia yake na Simba. Mola na aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUNZU AFIWA NA DADA YAKE, AENDA MSIBANI DRC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top