Tetesi za J'tano magazeti Ulaya


ROONEY AUZWA PAUNI MILIONI 40

Wayne Rooney anahofia Manchester United inajiandaa kumuuza kwa pauni Milioni 40. Na hofu hiyo inakuja baada ya kusajiliwa Robin van Persie kutoka Arsenal.
Theo Walcott
Walcott amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake na Arsenal na amekataa kusaini mkataba mpya
Winga wa England, Theo Walcott amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya Arsenal na anaweza kuuzwa kwa pauni Milioni 15 na klabu za Manchester City na Liverpool zipo mstari wa mbele kumsaini nyota huyo mwenye umri wa miaka 23.
Washambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na Nicolas Anelka wanaweza kuuzwa na klabu yao, Shanghai Shenhua kufuatia mgogoro unaoendelea kwenye klabu hiyo baina ya wanahisa wake.
Klabu ya Fenerbache ya Uturuki inaandaa dau la pauni Milioni 8 kumnunua kiungo wa Chelsea, Michael Essien na pia inataka kumchukua na mchezaji mwenzake Mreno, Raul Meireles.
Newcastle itakubali ofa za kuwauza beki Muargentina, Fabricio Coloccini, mwenye umri wa miaka 30, kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Cheick Tiote, mwenye umri wa miaka 26, au kiungo Mfaransa, Yohan Cabaye, mwenye miaka 26 pia.
Tottenham imeonywa inaweza kumkosa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Yann M'Vila mwenye umri wa miaka 22, baada ya dau la awali la pauni Milioni 12 kutaka kumnunua mchezaji huyo kupigwa chini,.
Kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas anataka kumsajili kiungo Mreno mwenye umri wa umri wa miaka 25, Moutinho kutoka Porto na mshambuliaji wa Urusi, Alan Dzagoev, mwenye umri wa miaka 22, kutoka CSKA Moscow, lakini anaweza kuwapoteza Jermain Defoe na Rafael van der Vaart.
Hamburg ya Ujerumani inatumai dau la pauni Milioni 9 litatosha kuinasa saini ya kiungo wa Tottenham, Van der Vaart mwenye umri wa miaka 29.
Wakala wa Dimitar Berbatov amekwenda Florence kufanya mpango wa uhamisho wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Bulgarian kutoka Manchester United kwenda Fiorentina.
Kocha wa Stoke City, Tony Pulis anatumai kufufua dili la kumsaini kwa mkopo kiungo wa Tottenham, Tom Huddlestone.

BRENDAN RODGERS AMRUDISHA BEKI STEWART DOWNING LIVERPOOL

Stewart Downing
Downing alitemwa kwenye kikosi cha kwanza Liverpool ikimenyana na Manchester City Jumapili
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amemuonya Stewart Downing kwamba winga huyo anaweza kurudishwa beki ya kushoto ili kupata nafasi ya kuendelea kuishi Anfield.
Kiungo wa Arsenal, Mikel Arteta ameelezea jinsi alivyochanganyikiwa na jinsi wachezaji wapya wanavyokabiliwa na changamoto ya kuchanganya haraka, baada ya kuondoka kwa nyota Robin van Persie.

REFA KITUKO BUNDESLIGA

Refa wa Ujerumani, alikuwa kituko katika mechi ya Bundesliga baina ya Hannover na Schalke baada ya chupa ya maji yake mwenyewe kumwagikia.