![]() |
| Mwili wa marehemu Kanumba |
JUMLA ya Sh. Milioni 53. 2 zilipatikana kutokana michango ya
msiba wa aliyekuwa nyota wa filamu Tanzania, Steven Charles Kanumba na Sh.
Milioni 52.1 zimetumika kwa gharama za msiba.
Kwa mujibu wa taarifa isiyo na mchanganuo, iliyotolewa leo
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Mazishi, Gabriel Mtitu ni
kwamba fedha zote zilizokusanywa ni Shilingi Milioni 53,252,000.Mtitu amesema katika fedha hizo zilizopatikana, ukitoa gharama za matumizi mbalimbali ambazo ni Shilingi 52, 102,000, zimebaki Shilingi Milioni 4, ambazo tayali amekabidhiwa Mama wa Marehemu Steve Kanumba.
Aidha, Mtitu amesema fedha zilizopatikana kwa michango ya M Pesa ni Shilingi 300,000 na kwenye Tigo Pesa ni Shilingi 150,000.
Jana baadhi ya vyombo vya habari nchini viliripoti kwamba Kamati ya Mazishi imechakachua fedha za michango.
Hata hivyo, taarifa ya Kamati hiyo, haitoi mchanganuo halisi wa mapato na matumizi zaidi ya kueleza idadi ya fedha zilizopatikana na zilizotumika.
Mbali na Mwenyekiti Gabriel Mtitu, watu wengine waliokuwepo kwenye Kamati hiyo ni Makamu Mwenyekiti, Jacob Steven ‘JB’, Katibu, William Mtitu na Wajumbe Issa Mussa ‘Cloud’ (Mweka Hazina), Kimosa na Vincent Kigosi ‘Ray’.
Wengine ni Single Mtambalike ‘Richie’, Dilesh Solanki, Millenne Happiness Magesse, Adele Kanumba (dada wa marehemu), Hartman Mblinyi, Ruge Mutahaba, Ally Choky, Simon Mwakifamba, Eric Shigongo, Steve Nyerere, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ na Mama Nassor, mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi Kanumba.



.png)
0 comments:
Post a Comment