ES Setif |
Wachezaji hao wametangaza mgomo huo ikiwa zimebaki saa
chache tu, kabla hawajacheza na Simba mechi ya pili ya hatua ya awali ya
michuano ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuchezwa kesho.
Gazeti la Habari Leo, limeandika kwamba Habari kutoka Algeria zinasema, nahodha wa timu hiyo Mourad
Delhoum aliyezungumza kwa niaba ya wenzake alisema taarifa hizo wameziwasilisha
kwa uongozi wa klabu hiyo.
Madai makubwa ya wachezaji hao mishahara yao pamoja na posho
za ligi ya ndani na michuano ya kimataifa ambapo walikumbusha kuwa waliwaonya
viongozi wao walipokuwa
Dar es Salaam kucheza na Simba wiki mbili zilizopita kwamba
wanataka walipwe fedha zao.
Na kwamba waliahidiwa wangelipwa fedha zao baada tu ya
kuwasili Algeria lakini mpaka juzi suala hilo halikuwepo.
Kiongozi wa timu hiyo, Hakim Serrar alikuwa safarini Algiers
kuhudhuria kikao cha viongozi wa klabu, lakini alilazimika kuahirisha safari
hiyo baada ya kuona kwenye vyombo vya habari kwamba wachezaji wameanza mgomo.
Kutokana na hilo, shughuli zote za klabu hiyo zilisimama
tangu juzi mpaka hapo uamuzi mwingine utakapotolewa na uongozi ulikuwa ukifanya
jitihada kuwalipa wachezaji chao.
Hata hivyo, viongozi wana muda mfupi sana kutafuta fedha kwa
ajili ya kulipa wachezaji wao kabla ya kukutana na Simba kesho na kama
hazitapatikana na wachezaji wakaendelea na mgomo wao kuna hatari ya kufungiwa
kushiriki michuano ya kimataifa kwa miaka miwili.
Hakim Serrar
hakufanya siri kulizungumzia hilo kama tatizo kubwa katika historia ya SSE, na
pia hakuficha kwamba wachezaji walikuwa na haki ya kufanya uamuzi waliofikia.
Simba iliondoka jijini Jumapili kuelekea Setif itakapochezwa
mechi hiyo kesho ambapo kabla ya kuelekea Algeria kwanza walilala Cairo, Misri
na Jumanne kuelekea Setif.
0 comments:
Post a Comment