• HABARI MPYA

    Thursday, April 05, 2012

    NI BARCELONA NA CHELSEA, REAL NA BAYERN NUSU FAINALI ULAYA

    Meireles akishangilia bao lake
    Real wakishangilia
    KLABU ya Chelsea usiku huu imeifunga Benfica ya Ureno mabao 2-1, wafungaji Frank Lampard na Raul Meireles na kufuzu kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.
    Kwa ushindi huo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Chelsea ya England sasa itakutana na mabingwa watetezi, Barcelona ya Hispania kwenye Nusu Fainali.
    Katika mchezo mwingine, Real Madrid ya Hispania imeshinda mabao 5-2 dhidi ya APOEL Nicosia ya Cyprus, Cristiano Ronaldo akifunga mabao mawili na kutimiza mabao 49 msimu huu.
    Real sasa imetinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 8-2 na itakutana na Bayern Munich ya Ujerumani katika Nusu Fainali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI BARCELONA NA CHELSEA, REAL NA BAYERN NUSU FAINALI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top