Lulu mahakamani leo |
Muigizaji wa Filamu nchini
anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth
Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana
na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.
Elizabeth Michael amesomewa
mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya
mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko
sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.
Elizabeth Hakutakiwa kujibu
chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za
mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa na
kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.
Muigizaji huyo aliletwa
mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia
ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi
alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa
katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T
848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.
SOURCE: Mtaa kwa mtaa Blog
0 comments:
Post a Comment