• HABARI MPYA

  Monday, April 03, 2017

  ONYANGO NAHODHA MPYA UGANDA BAADA YA MASSA KUSTAAFU

  KIPA wa kwanza wa Uganda Cranes, Denis Onyango ameteuliwa kuwa Nahodha mpya wa timu hiyo kufuatia kustaafu kwa Geoffrey Massa Jumatano iliyopita.
  Kocha wa Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic amesema kwamba uzoefu na hekima za Onyango ndizo zimemfanya ampe uongozi wa wachezaji wenzake katika timu.
  “Onyango atakuwa Nahodha mpya wa Uganda Cranes kwa sababu ya uzoefu wake, utu uzima, tabia, uongozi na vigezo vingine vyote,” alisema Micho.
  Kipa huyo wa Mamelodi Sundowns alipewa kitambaa katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ghana mjini Tamale Oktoba mwaka jana na akaisaidia Cranes kupata sare ya ugenini dhidi ya kikosi imatra cha Black Stars.
  Denis Onyango ndiye Nahodha mpya wa Uganda baada ya Geoffrey Massa kustaafu Jumatano iliyopita

  Onyango atasaidiwa na mchezaji mwingine mzoefu, Hassan Wasswa ambaye alikuwa Nahodha wa Cranes dhdi ya Mali nchini Uganda kwenye mchezo wa Kundi D Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 mjini Oyem, Gabon baada ya Massa kuanzia benchi na katika mchezo wa kirafiki wa sare na Kenya mjini Machakos.
  Onyango alikuwa mwaka mzuri uliopita, akiiwezesha Uganda kufuzu Afcon 2017 baada ya miaka 39 na kuipa Mamelodi mataji matatu likiwemo la Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini na Kombe la Telkom.
  Kutokana na mafanikio hayo, haikuwa ajabu Onyango akashinda tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, akiweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kushinda hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ONYANGO NAHODHA MPYA UGANDA BAADA YA MASSA KUSTAAFU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top