• HABARI MPYA

    Monday, November 07, 2016

    LWANDAMINA KUTUA DAR JUMATANO KUANZA KAZI RASMI YANGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina anatarajiwa kutua nchini Jumatano baada ya kumalizana na klabu yake ya sasa, Zesco United ya kwao.
    Issued  by 
    Kwa pamoja, Justin Mumba na Katebe Chengo Mtendaji Mkuu wa ZESCO na Ofisa Habari wametoa taarifa ya kuachana na Lwandamina.
    Lwandamina ambaye amekwishamalizana na uongozi wa Yanga jana aliiongoza Zesco United katika mechi ya Ligi Kuu ya Zambia dhidi ya Nkana FC na leo anatarajiwa kuwa na kikao na waajiri wake.
    George Lwandamina anatarajiwa kutua nchini Jumatano kujiunga rasmi na Yanga 

    “ZESCO United FC inapenda kutangaza kwamba Kocha Mkuu, George Lwandamina asubuhi hii amewasilisha barua ya kujiuzulu mara moja. Klabu imeafiki kujiuzulu kwake na inapenda kumshukuru kwa kazi na mchango wake alipokuwa kazini," wamesema.
    Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa kocha Hans van der Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
    Hata hivyo, mpango huo unakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wadau wa timu hiyo na wapenzi wanaoamini Pluijm bao chaguo sahihi Jangwani.
    Ikumbukwe wiki mbili zilizopita Pluijm alisusa kwa siku tatu kufanya kazi Yanga na kuwasilisha barua ya kujiuzulu baada ya kukerwa na taarifa za ujio wa Lwandamina.   
    Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliingilia kati suala hilo na kufanikiwa kumrejesha kazini Pluijm. Waziri Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, kwanza aliushauri uongozi kumrudisha Pluijm na baadaye akaenda kuzungumza na kocha huyo pia kumshauri akubali kurejea.
    Baadaye akazikutanisha pande zote mbili, Pluijm na uongozi wa Yanga katika kikao ambacho inaelezwa makubaliano yalifikiwa kabla ya uongozi wa Yanga kumemuandikia barua Mholanzi huyo kumuomba radhi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LWANDAMINA KUTUA DAR JUMATANO KUANZA KAZI RASMI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top