• HABARI MPYA

  Wednesday, November 09, 2016

  LWANDAMINA AWASILI KIMYA KIMYA DAR TAYARI KUANZA KAZI YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amewasili mjini Dar es Salaam jioni ya leo tayari kusaini mkataba wa kazi na mwajiri mpya.
  Lwandamina anatua nchini baada ya kumalizana na klabu yake, Zesco United ya kwao aliyoifanyia kazi tangu mwaka 2014.
  Hata hivyo, kuna uwezekano Lwandamina akaishuhudia kwenye Televisheni mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho kati ya Yanga na Ruvu Shooting.
  Na hiyo ni kwa sababu uongozi wa Yanga unafikiria utamkosesha raha kocha anayemaliza muda wake, Mholanzi Hans van der Pluijm.
  George Lwandamina anatarajiwa kutua nchini Jumatano kujiunga rasmi na Yanga 

  "Hatutaki kumnyima raha Babu (Pluijm). Tunafikiria Lwandamina abaki tu hotelini aangalie mechi kwenye Televisheni na baada ya hapo atapatiwa DVD za mechi nyingine zilizopita ili kuijua timu vizuri,"kimesema chanzo kutoka Yanga leo.
  Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa kocha Hans van der Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AWASILI KIMYA KIMYA DAR TAYARI KUANZA KAZI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top