• HABARI MPYA

  Wednesday, November 09, 2016

  CAF YABORESHA ZAWADI MICHUANO YA AFRIKA

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeboresha zawadi za mashindano ya klabu na timu za taifa katika michuno yake mbalimbali kuanzia mwaka 2017 hadi 2019.
  Hatua hiyo inafuatia kikao kilichofanyika Septemba 27, mwaka huu mjini Cairo, Misri.
  Taarifa kutoka makao makuu ya CAF, Mtaa wa Abdel Khalek Tharwat mjini El Hay El Motamayez, Misri imesema kwamba maboresho hayo yanahusu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa fainali za 2017 na 2019, Fainali mbili zijazo za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa miaka miwili ijayo.
  Ikumbukwe CAF imeongeza idadi ya timu za kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabinhgwa kutoka nane hadi 16.) GONGA KUONA ZAWADI MPYA   • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YABORESHA ZAWADI MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top