• HABARI MPYA

    Friday, November 18, 2016

    AZAM FC WATAKA KUMSAJILI KABUNDA WA MWADUI FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    AZAM FC inataka kuboresha zaidi kikosi chake kwa kumsajili winga wa Mwadui FC ya Shinyanga, Hassan Kabunda.
    Na tayari Mwadui wameshitukia mpango huo na leo wametoa onyo kwa timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake. 
    Kocha wa Mwadui FC, Khalid Adam ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba Azam FC wanapaswa kufuata taratibu kama wanamtaka Kabuda.
    Hassan Kabunda (kulia) yupo kwenye rada za Azam FC, timu inayomilikiwa na bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake 

    “⁠⁠Kabunda bado ana mkataba na Mwadui. Hivyo kama Azam wanamtaka, wake kuzungumza na sisi, huo ndiyo utaratibu,”amesema.
    Mtoto huyo wa beki wa zamani wa kimataifa wa Yanga, Salum Kabunda aliyevuma kwa majina ya utani ya Ninja na Msudan (sasa marehemu) ni kati ya wachezaji wanaofanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara tangu msimu uliopita.
    Na mchezaji huyo wa zamani wa Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam mapema msimu huu alikaribia kusajiliwa na Simba SC kama si kushindwana dau.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WATAKA KUMSAJILI KABUNDA WA MWADUI FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top