• HABARI MPYA

  Saturday, October 08, 2016

  UGANDA WALAZIMISHA SARE UGENINI GHANA, 0-0

  TIMU ya taifa ya Uganda imelazimisha sare ya 0-0 na wenyeji Ghana maarufu kama Black Stars katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Uruei uliofanyika Ijumaa Uwanja wa Tamale.
  The Cranes walionyesha kiwango kizuri ukiwa mwendelezo wa kuwapa raha Waganda baada ya kufuzu Fainali za Kombe la TOTAL Afrika nchini Gabon 2017 wakitumia mchezo wa kujihami kwa nidhamu ya hali ya juu.
  Sifa zimuendee kipa wa The Cranes inayofundishwa na Mserbia, Milutin 'Micho' Sredojevic, Denis Onyango anayedakia klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa kuokoa michomo mingi ya hatari.
  Na Wageni walikaribia kupata bao dakika ya 20 wakati Khalid Aucho aliposhindwa kumaliza kazi nzuri ya Farouk Miya.
  Jordan Ayew, Nahodha Asamoah Gyan na Christian Atsu baadaye wote wakapoteza nafasi nzuri za kuifungia Ghana.
  Kongo itakuwa mwenyeji wa Misri katika mchezo mwingine wa ufunguzi wa Kundi E Jumapili mjini Kintele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA WALAZIMISHA SARE UGENINI GHANA, 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top