• HABARI MPYA

  Thursday, October 13, 2016

  TYSON APOKONYWA LESENI YA NDONDI BAADA YA KUMKACHA KLITSCHKO

  BODI ya Ndondi Uingereza (BBBofC) imesimamisha leseni ya bondia Tyson Fury baada ya jana usiku kuvua mikanda ya ubingwa wa dunia ya WBO na WBA jana usiku na kujitoa kwenye pambano la Wladimir Klitschko.
  Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa BBBofC, bodi hiyo imethibitisha kufungia leseni ya Fury hadi hapo uchunguzi utakapokamilika juu ya vipimo vya utumiaji wa dawa za kulevya na matibabu yake.
  Bondia huyo mkorofi, hivi karibuni alijitoa kwenye pambano la marudiano na Wladimir Klitschko kwa mara ya pili mfululizo baada ya taarifa ya kitabibu kusema hayuko fiti, iliyotanguliwa na taarifa za kubainika anatumia dawa za kulevya aina ya cocaine.
  Tyson Fury amepokonywa leseni ya kupigana baada ya kuvua mikanda ya ubingwa wa dunia ya WBO na WBA jana usiku

  Tangazo la Fury kuvuliwa mikanda ya ubingwa linaashiria ujio wa pambano kati ya Klitschko na Anthony Joshua kuwania mataji hayo ambayo sasa yako wazi. 
  Promota Eddie Hearn awali alisema kwamba pambano la Joshua na Klitschko linaweza kuwapo tu kama kutakuwa na mkanda mwingine wa ubingwa wa kugombea.
  Katika taarifa yake, bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema: "Nilishinda mataji hayo ulingoni na naamini ninapaswa kuyapoteza ulingoni, lakini siko tayari kuyatetea kwa wakati huu na nimechukua maamuzi magumu na ya kuudhi kuyavua rasmi sasa mataji yangu ya dunia na ninawatakia kila heri washindani wengine watakaoyawania wakati huu ninakabaliana na changmoto nyingine kubwa katika katika maisha yangu, ambayo ninajua, kama Klitschko, nitayashinda,". 
  Fury aliushangaza ulimwengu kwa kumpiga mbabe wa Ukraine, Klitschko Novemba mwaka 2015 na kutwaa pia taji la IBO, lakini mara mbili akajitoa kwenye pambano la kutetea mataji yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON APOKONYWA LESENI YA NDONDI BAADA YA KUMKACHA KLITSCHKO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top