• HABARI MPYA

  Sunday, October 16, 2016

  TAMBWE NJE KABISA YANGA NA AZAM, WANAANZA CHIRWA NA NGOMA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  TEGEMEO la mabao la Yanga, Amissi Joselyn Tambwe hayumo kabisa katika mpango wa mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Mrundi huyo aliumia katika mchezo uliopita Yanga ikishinda 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro baada ya kugongana na Nahodha wa wapinzani, Shaaban Nditi dakika ya 87 na kushindwa kuendelea na mchezo.
  Dawati la tiba la Yanga lilijaribu kupambana kumrejesha uwanjani mapema, lakini imeshindikana na leo kocha Mholanzi amewaanzisha pamoja wachezaji wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe, Donald Ngoma na Obrey Chirwa mbele ya lango la Azam.
  Obrey Chirwa ameanzishwa pamoja na Ngoma leo dhidi ya Azam FC

  Mzambia Chirwa na Mzimbabwe Ngoma wote walifunga katika ushindi wa 3-1 kwenye mchezo uliopita na leo Pluijm anajaribu tena kushuhudia matunda ya uwili wao.
  Kikosi cha Yanga leo ni; Deo Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew, Kelvin Yondan, Saidi JUma 'Makapu', Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Deus Kaseke.
  Katika benchi watakuwapo Beno Kakolanya, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Matheo Anthony, Mbuyu Twite, Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAMBWE NJE KABISA YANGA NA AZAM, WANAANZA CHIRWA NA NGOMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top