• HABARI MPYA

  Wednesday, October 12, 2016

  PLUIJM AWAPIGA BENCHI NGOMA, TWITE AWAANZISHA CHIRWA NA MAKAPU LEO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amemuanzisha winga Mzambia Obrey Chirwa katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar leo, huku akimuanzishia benchi mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma.
  Yanga watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Winga Mzambia Obrey Chirwa anaanza leo dhidi ya Mtibwa Sugar

  Na katika mchezo huo, kocha Pluijm amefanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi chake cha kwanza akiwapumzisha kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, kiungo Mkongo Mbuyu Twite na Ngoma, akiwaingiza Deo Munishi ‘Dida’ langoni, Said Juma Makapu kiungo wa ulinzi na Chirwa kucheza mshambuliaji pacha wa Mrundi, Amissi Tambwe.
  Kwa ujumla kikosi cha Yanga leo ni; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Vincent Andrew, Kevin Yondan, Said Makapu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke,
  Katika benchi watakuwapo; Beno Kakolanya, Matheo Antony, Pato Ngonyani, Juma Mahadhi, Geofrey Mwashuiya, Mbuyu Twite na Donald Ngoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AWAPIGA BENCHI NGOMA, TWITE AWAANZISHA CHIRWA NA MAKAPU LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top