• HABARI MPYA

  Friday, October 07, 2016

  PAMBA NA POLISI DAR KESHO KAZI IPO KIRUMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Daraja la Kwanza Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa mechi za Kundi A kati ya wenyeji, Pamba SC na Polisi ya Dar es Salaam Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, wakati African Sports itakuwa mwenyeji wa Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
  Ligi hiyo ya Daraja la Kwanza itaendelea Jumapili Oktoba 9, 2016 kwa mchezo utakaozikutanisha Ashanti United na Friends Rangers; zote za Dar es Salaam. Kadhalika Jumatatu, kutakuwa na mchezo kati ya Mshikamano ya Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa. Mchezo huo, pia utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
  Kundi B; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Kurugenzi ya Iringa na Coastal Union ya Tanga ufakaofanyika huko Mufindi ukifuatiwa na michezo mitatu siku ya Jumapili Oktoba 9 ambayo Mlale itacheza na Polisi Moro huko Uwanja wa Majimaji, mjini Songea wakati Njombe Mji itaikaribisha Kemondo wakati KMC itacheza na Mbeya Warriors kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
  Kundi C; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu Mvuvumwa ya Kigoma itacheza na Singida United ya Singida wakati Panoni itapambana na Alliance huku Polisi Dodoma itacheza na Polisi Mara wakati Jumapili Rhino ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT ya Tanga.Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Oktoba 8, 2016 kwa michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
  Wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam JKT Ruvu yenyewe itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMBA NA POLISI DAR KESHO KAZI IPO KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top