• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2016

  MANJI AKUTANA NA VIONGOZI WA MATAWI LEO JANGWANI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji mchana wa leo atakuwa na kikao na viongozi wa matawi ya klabu hiyo mjini Dar es Salaam.
  Kikao hicho kitafanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na bila shaka Manji atakuwa anazungumzia msimamo wake juu ya sakata la kuikodisha timu kwa miaka 10.
  Kikao hicho kitafanyika kabla ya Mkutano Mkuu wa dharula wa wanachama wote uliopangwa kufanyika Jumapili ya Oktoba 23, mwaka huu katika ukumbi ambao utatajwa baadaye.
  Manji mchana wa leo atakuwa na kikao na viongozi wa matawi ya Yanga Jangwani

  Kikao cha leo kinafuatia Baraza la Wadhamini la Yanga SC kuikodisha timu ya soka kwa kampuni ya Yanga Yetu, inayomilikiwa na Mwenyekiti huyo wa klabu, Manji ambayo itakuwa mmiliki wa klabu kwa miaka 10 ijayo.
  Na hatua ya Baraza ilifuatia azimio la wanachama wa klabu hiyo Agosti 6, katika Mkutano mwingine wa dharula pia kukubali kumkodisha klabu hiyo kiongozi wao huyo mkuu kwa miaka 10.
  Manji aliomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.
  Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini yake Manji. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANJI AKUTANA NA VIONGOZI WA MATAWI LEO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top