• HABARI MPYA

    Friday, October 07, 2016

    BABU NGASSA AANZA VYEMA TOTO, YAILAZA KAGERA SUGAR 2-0 BUKOBA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA mpya wa Toto Africans ya Mwanza, Khalfan Ngassa ‘Babu’ ameanza vyema baada ya kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo.
    Pongezi kwao wafungaji wa mabao hayo, Jamal Soud dakika ya 47 na Mohamed Soud dakika ya 80, waliomtungua kipa wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, Hussein Sharrif ‘Casillas’.
    Khalfan Ngassa ‘Babu’ (kushoto) akiwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Pamba na Simba, Juma Amir Maftah  

    Huo ulikuwa mchezo wa kwanza Toto ikicheza chini ya kocha mpya, Khalfan Ngassa baada ya kuondolewa kwa Rogasian Kaijage aliyekuwa kocha wa timu tangu mwanzo wa msimi baada ya kuondolewa kwa John Tegete.
    Kwa matokeo hayo, Toto inafikisha point inane baada ya kucheza mechi nane, huu ukiwa mchezo wa pili kushinda baada ya kufungwa mechi nne na kutoa sare mbili.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BABU NGASSA AANZA VYEMA TOTO, YAILAZA KAGERA SUGAR 2-0 BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top