SERENGETI BOYS NA BLACK STARLETS KATIKA PICHA JANA TAIFA
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Assad Juma (kulia) akimtoka Lavesh Gabriel wa Ghana, Back Starlets katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2
Kiungo wa Tanzania, Shaaban Zubeiry Ada (katikati) akimdhibiti kiungo wa Ghana, Lavesh Gabriel (kushoto)
Kiungo wa Tanzania, Abdallah Rashid (kulia) akitafuta maarifa ya kuwapita wachezaji wa Ghana
Beki wa Tanzania, Nickson Kibabage akimlamba chenga mchezaji wa Ghana
Shaaban Zubeiry wa Serengeti Boys akipiga mpira mbele ya Lavesh Gabriel wa Ghana
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harison Mwakyembe akizungumza wakati wa kukabidhi bendera ya taifa kwa wachezaji wa Serengeti Boys ambao Jumatano wanakwenda Morocco kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa fainali za Mataifa ya Afrika nchini Gabin mwezi ujao
Waziri Mwakyembe (kulia) akimkabidhi bendera Nahodha wa Serengeti Boys, Ally Msengi (katikati) na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi waliohudhuria mchezo wa jana
Kikosi cha jana kilichoanza mechi ya jana na kikosi ni kikosi cha Tanzania
Ogun donates land to FG to develop inland dry port
-
From Idu Jude, Abuja The Government of Ogun State has donated over 130
hectares of land to the federal government of Nigeria for the development
of an in...
0 comments:
Post a Comment