• HABARI MPYA

    Wednesday, April 12, 2017

    MBEYA CITY UWANJANI KESHO

    Na Steven Kinabo, DAR ES SALAAM
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kwa timu ya Mbeya City kuikaribisha African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kuanza Saa 10.00 jioni.
    Ligi itaendele Jumamosi kwa michezo mine, Stand United wakiwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na Toto Africans wakiikaribisha Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
    Mrisho Ngassa ataiongoza Mbeya City dhidi ya African Lyon kesho 

    Mechi nyingine za Jumamosi, Majimaji ya Songea itaifuata Ruvu Shooting  Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani - mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana wakati JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
    Kwa mujibu wa ratiba, Jumapili Mbao watacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza huku Mwadui wakiwa wenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Mwadui, Shinyanga. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY UWANJANI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top