• HABARI MPYA

    Thursday, November 10, 2016

    YANGA YAPATA UONGOZI RASMI BUNGENI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Yanga leo imepata uongozi wa muda ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi uliofanyika Bungeni mjini Dodoma.
    Katika uchaguzi huo, Venance Mwamoto alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu wake Ridhiwani Kikwete, Katibu Mkuu Hafidh Ally Tahir, Naibu wake Hamidu Bobali, Mweka Hazina Martha Mlata na Msaidizi wake Abdallah Ulega.
    Waliochaguliwa nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Grace Kihwelu, Halima Mdee, Seif Gulamali, Gibson Meiseyeki, Issa Mangungu na Dotto Biteko.
    Ridhiwani Kikwete (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo, Makamu Mwenyekiti, Ridhiwani Kikwete alisema kwamba uongozi huo wa muda ambao utakuwa na jukumu la kuandaa mchakato kamili wa uundwaji wa tawi la Yanga Bungeni.
    Kikwete alisema kwamba uongozi pia umeteua Baraza la Wadhamini ambalo litaundwa na Freeman Mbowe, Mwigulu Nchemba na Hawa Ghasia wakati Mjumbe mwingine mmoja mmoja atatoka Zanzibar.   
    "Kwa muda kumekuwa na Wabunge wenye mapenzi na Yanga, hata kabla ya sisi kuingia. Lakini safari hii tumeamua kuunda tawi la rasmi la Yanga bungeni, ambalo sifa ya kuwa mwanachama wake ni uwe Mbunge,"alisema Kikwete. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAPATA UONGOZI RASMI BUNGENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top