WAPINZANI wa England katika Kundi D Kombe la Dunia, Uruguay wameifunga Slovenia mabao 2-0 usiku wa jana.
Uruguay ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa Edinson Cavani aliyeunganisha krosi ya Diego Forlan dakika ya 37 mjini Montevideo.
Bao la pili la Uruguay lilifungwa na Cristian Stuani zikiwa zimesalia dakika 14 mchezo huo kumalizika. Wakati huo huo mshambuliaji majeruhi wa timu hiyo, Luis Suarez amepiga picha ya kikosi cha wachezaji wote wa timu hiyo kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka huu. Uruguay itaanza na Costa Rica Juni 14 mjini Fortaleza.
Kikosi kamili: Luis Suarez hayuko fiti, lakini jana alipiga picha ya pamoja ya kikosi cha timu hiyo cha Kombe la Dunia
0 comments:
Post a Comment