// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI D LENYE ENGLAND, ITALIA NA URUGUAY WOTE MABINGWA WA ZAMANI, NANI ATAKWAMA? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI D LENYE ENGLAND, ITALIA NA URUGUAY WOTE MABINGWA WA ZAMANI, NANI ATAKWAMA? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, June 07, 2014

    KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI D LENYE ENGLAND, ITALIA NA URUGUAY WOTE MABINGWA WA ZAMANI, NANI ATAKWAMA?

    ENGLAND ipo kundi moja na Italia, Uruguay na Costa Rica katika Kombe la Dunia.
    BIN ZUBEIRY inaendelea kukuletea makala za mchambuzi na beki wa zamani wa Three Lions, Martin Keown haps akilichambua Kundi D.

    Tegemeo: Wayne Rooney ataiongoza England katika Kombe la Dunia Brazil
    Kundi D
    England
    Uruguay
    Italia
    Costa Rica
    Utabiri wa Keown;
    1 Italy
    2 England
    3 Uruguay
    4 Costa Rica
    Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
    Jun 14        Uruguay v Costa Rica  Saa 4:00 usiku Fortaleza
    Jun 14        
    England v Italia             Saa 7:00 usiku  Manaus
    Jun 19        
    Uruguay v England       Saa 4:00 usiku S. Paulo
    Jun 20        
    Italia v Costa Rica        Saa 1:00 usiku Recife
    Jun 24        
    Italia v Uruguay            Saa 1:00 usiku Natal
    Jun 24        
    Costa Rica v England  Saa 1:00 usiku Horizonte
    URUGUAY
    Viwango vya FIFA: Namba 7
    Kocha: Oscar Tabarez. Katika awamu yake ya pili ya kuifundisha Uruguay ameshinda michuano mikubwa na akashika nafasi ya nne katika michuano mingle mitatu.
    Nahodha: Diego Lugano (West Brom)
    Mchezaji wa kumulikwa: Edinson Cavani (PSG) kwa klabu yake na timu yake ya taifa Cavani hupangwa pembeni, lakini kuumia kwa Luis Suarez anayepatiwa matibabu ya goti kliniki nchini Brazil, kunaweza kumfanya apangwe katikati. Cavani hakika ni bidhaa adimu.
    Bring it on: Edinson Cavani will have an even heavier workload if Luis Suarez fails to get over his injury
    Mtupe ndani: Edinson Cavani anaweza kuchezwa kama mshambuliaji wa kati baada ya Luis Suarez kuumia

    Ubora wao: Hawakati tamaa. Suarez hakuona tatizo kuuzuia kwa mkopo mpira mwaka 2010 katika Robo Fainali dhidi ya Ghana kuizuia timu hiyo ya Afrika kupata bao la ushindi na mchezi kuhamia Kenya penalti, ambako Uruguay ilishinda.
    Hatari: Kukaa na mpira. Uruguay wanatumia mchezo wa kujihami zaidi huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza,a mfumo ambao unaendana sana na aina ya vipaji ilivyonavyo. 
    Watakwenda England? Diego Godin ni miongoni mea wachezaji wanaotakiwa Chelsea, wakati Cavani anatakiwa na Manchester United. Abel Hernandez wa Palermo pia anatakiwa England.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi (1930 na 1950)
    Walivyofika hapa: Walishika nafasi ya tank Amerika Kusini na kuifunga Jordan 5-0 katika mechi mvili za mchujo kuwania tiketi ya Brazil. 
    Je, wajua: Tabarez alikuwa pia kocha wa Uruguay wakati wa Kombe la Italia mwaka 1990. Aliifikisha Uruguay hatua ya mtoano, ambako ilitolewa na Italia 16 Bora.
    ENGLAND  
    Viwango vya FIFA: Namba 10
    Kocha: Roy Hodgson. Hana mzigo wa lawama za matarajio, lakini amedhamiria kufanya kitu Brazil.
    Nahodha: Steven Gerrard (Liverpool)
    Mchezaji wa kumulikwa: Raheem Sterling (Liverpool). Alimaliza msimu vizuri akiwa katika kiwango cha juu Liverpool na ni mmoja wa wachezaji bora chipukizi Ulaya. Inaonekana kama Hodgson anaweza kumtumia kama mchezaji muhimu wa kutokea benchi kwenda kubadilisha au kuongeza nguvu kwenye timu. Ni vigumu kumdhibiti kwa sababu ni vigumu kumsoma na kasi yake, uwezo wa kupiga chenga na kuwatoka mabeki vinaweza kusababisha matatizo kwa wapinzani wowote.
    Unleashed: Youngster Ross Barkley impressed in England's friendly draw with Ecuador in Miami
    Kifaa: Kinda Ross Barkley alikuwa kivutio katika mchezo wa kirafiki wa England na Ecuador ulioisha kwa sare Miami

    Ubora wao: Hawafungiki kwa urahisi. England ilifungwa mabao manne katika mechi za kufuzu na kucheza mechi sita bila nyavu zao kutikiswa chini ya kocha Hodgson. 
    Hatari: Kucheza kama timu. England imekuwa na wachezaji mafundi na wabunifu, lakini kwa miaka kadhaa imewawia vigumu kuwa na muunganiko wenye madhara kwa wapinzani. Sasa watatazamwa Brazil kama wamebadilika. 
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi (1966)
    Walivyofika hapa: Waliongoza Kundi H kwenye mechi za kufuzu baada tu ya kushinda mechi mbili za mwisho. Waliifunga Ukraine kupaa kileleni mwa kundi kwa pointi moja.
    Je, wajua? Licha ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti kwenye Fainali tatu za Kombe la Dunia (saws na wapinzani wao kwenye kundi hilo, Italia), England haijawahi kukosa penalti Kombe la Dunia katika muda wa kawaida wa mchezo. Walifunga mikwaju yote saba waliyopata.
    ITALIA
    Viwango vya FIFA: Namba 9
    Kocha: Cesare Prandelli. Aliiwezesha Italia kufuzu Kombe la Dunia ikiwa na mechi mbili mkononi – kwa mara ya kwanza katika hisoria yao.
    Nahodha: Gianluigi Buffon (Juventus)
    Mchezaji wa kumulikwa: Mario Balotelli (AC Milan). Balotelli alitisha katika Euro 2012 wakati alipoibuka mshambuliaji mgumu kumdhibiti mmoja mmoja. Ikiwa atarejea na makali hayo hayo, hatakuwa tu mshambuliaji tegemeo wa Italia, bali pia nyota wa mashindano yote.
    Super Mario: Balotelli will be looking to give England's defence a torrid time in Italy's opening game
    Super Mario: Balotelli anatarajiwa kuipa wakati mgumu safu ya ulinzi ya England katika mchezo wa ufunguzi wa Italia

    Ubora wao: Mseto wa chipukizi na wazofu. Wakongwe kama Buffon na Andrea Pirlo wanafiti kabisa pamoja na chipukizi wenye vipaji kama Marco Verratti na Stephan El Shaarawy.
    Hatari: Kurudia yaliyopita. Italia haijawahi kuwa na safu dhaifu ya ulinzi, lakini hii The Azzurri ya sasa inakosa mamlaka kama ile ya zamani. 
    Atakwenda England? Balotelli ni nyota anayeivutia Arsenal na zaidi - anaweza kumpita beki yeyote.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi (1934, 1938, 1982 na 2006)
    Walivyofika haps: Walifuzu kiulaini kutoka Kundi B wakiizidi pointi sita, Denmark iliyoshika nafasi ya pili.
    Je, wajua? Buffon atakuwa anacheza Fainali zake za tano za Kombe la Dunia, akiwa mchezaji wa tatu tu kufanya hivyo baada ya Antonio Carbajal wa Mexico na Lothar Matthaus wa Ujerumani
    COSTA RICA 
    Viwango vya FIFA: Namba 28
    Kocha: Jorge Luis Pinto. Mcolombia huyo alimwaga machozi akihojiwa na kituo cha Redio katika usiku ambao  Costa Rica ilifuzu Kombe la Dunia.
    Nahodha: Bryan Ruiz (Fulham) 
    Mchezaji wa kumulikwa: Joel Campbell (Arsenal). Tuliona vita vya mshambuliaji huyo kwenye Ligi ya Mabingwa wakati alipokuwa akicheza kwa mkopo Olympiacos. Sasa amepata fursa ya kutumia kasi yake na mbinu kuionyesha dunia nini anaweza kufanya.
    Ubora wao: Kupaki basi. Pinto anapenda kucheza na mabeki watatu wa kati na mabeki wake wa pembeni wanasogea mbele. Na kwa kujaza viungo katikati, inawatengenezea ugumu wao wenyewe kupasua ngome za wapinzani.
    Hatari: Mchezo wa kujihami. Pinto hapendi kuwaruhusu wachezaji wake kusogea mbele na kipaumbele chake cha kwanza na kuwa na timu ngumu kufungika, ambayo inaeleweka kwenye kundi gumu. 
    Atakwenda England? Alvaro Saborio anaweza kuwa mchezaji anayefuatiliwa na was aka vipaji, lakini Keylor Navas ana uamuzi wa kurejea Ligi Kuu England akawe mamba moja.
    Matokeo mazuri kombela Dunia: 16 Bora (1990)
    Walivyofika hapa: Walimaliza nyuma ya Mexico katika hatua ya kwanza ya kundi, lakini baadaye wakawa wa pili katika hatua ya mwisho ya kundi la timu sita, nyuma ya Marekani hivyo kufuzu. 
    Je, wajua? Kocha Pinto ni pasha kichwa mno. Mwaka 2009 alifungiwa mechi10 baada ya kumtukana na kumsukuma refa wa akiba katika mchezo wa klabu Colombia. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI D LENYE ENGLAND, ITALIA NA URUGUAY WOTE MABINGWA WA ZAMANI, NANI ATAKWAMA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top