Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba Alex Song anaweza kumfuatia Robin van Persie kuondoka katika klabu hiyo.
Song amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kuhamia Barcelona, na inasemekana Wenger atakuwa bila kiongozi nyota kwenye msimu mpya. Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kusajili zaidi, kama na Song akiondoka pia, Wenger alisema: 'Yote yanawza kutokea'.
Alex Song (kushoto) katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya na Arsenal
Wenger amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo asubuhi kwamba bado hakuna ombi rasmi la Barcelona kwa ajili ya Song.
Kocha huyo wa muda mrefu Arsenal, kwa mara nyingine ametetea uamuzi wake wa kumuuza Van Persie kwa wapinzani wake wakubwa, Manchester United. Mholanzi huyo alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, na mashabiki wengi wamekasirishwa na kitendo cha klabu kumuuza tena mmoja wa nyota wake baab kubwa.
Van Persie amesaini mkataba wa pauni Milioni 12 kwa mwaka na United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alipelekwa kwenye Uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo leo asubuhi, kusaini mkataba wa mshahara mnono wa pauni 250,000 kwa wiki, ambao utamfanya yeye Wayne Rooney wawe wachezaji wanaolipwa zaidi Man United.
Njiani kuondoka? Alex Song akiichezea Arsenal dhidi ya Manchester City mjini Beijing mwezi uliopita
Wenger amemteua Thomas Vermaelen kuwa Nahodha mpya, wakati Mikel Arteta atakuwa Msaidizi wake.
Arsenal itaanza kampeni yake ya kuwania taji la Ligi Kuu nyumbani na Sunderland kesho. Klabu mbili za Manchester zinatarajiwa kutawala tena, lakini Wenger amewaambia Waandishi wa Habari The Gunners wako vizuri katika mbio za taji, ingawa hawatabiriwi.
Vigogo hao wa London hawajashinda taji la Ligi Kuu tangu mwaka 2004 na taji lao la mwisho kwa ujumla walipata Kombe la FA mwaka 2005.
Nahodha mpya: Thomas Vermaelen amechukua nafasi ya Robin Van Persie
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk


.png)
0 comments:
Post a Comment