• HABARI MPYA

    Wednesday, August 15, 2012

    COASTAL YAFUNGWA TATU IKIFUNGA MBILI MOMBASA

    Coastal Union; wamefungwa 3-2 Mombasa

    Na Prince Akbar
    BANDARI ya Mombasa, Kenya inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo, jioni hii imeifunga mabao 3-2 Coastal Union ya Tanga inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, katika mchezo wa kirafiki, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbarak Sports, Mombasa.
    Bandari walitangulia kupata bao lililofungwa na Nahodha wao kabla ya Nsa Job kuisawazishia Coastal Union kwa penalti pia.
    Bandari wakafunga bao la pili kupitia kwa Shaaban Kenga, lakini mshambuliaji wa zamani wa Simba, Yanga, Azam na Moro United, Nsa Job akasawazisha tena kwa penalty na hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana 2-2.
    Bandari ilipata bao lake la ushindi kupitia kwa Erick Okoth na jitihada za mabingwa wa Bara 1988 kusaka bao la kusawazisha ziligonga mwamba.
    “Mchezo ulikuwa mzuri, wenye ushindani, Coastal wamerudi Tanga baada ya mechi, sisi tunasafiri kuelekea Nairobi kwa ajili ya mechi ya Jumamosi ya Ligi na Iron Strikers,” alisema beki wa Bandari, Mtanzania, David Naftali alipozungumza na BIN ZUBEIRY kutoka Mombasa jioni hii.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL YAFUNGWA TATU IKIFUNGA MBILI MOMBASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top