• HABARI MPYA

    Thursday, June 07, 2012

    MAN CITY KUMSAJILI STURRIDGE


    EPL: Daniel Sturridge, Tottenham Hotspur v Chelsea
    Sturridge

    KLABU ya Manchester City inajiandaa kumsajili Daniel Sturridge wa Chelsea kwa dau la pauni Milioni 10, ikitumia mwanya wa mchezaji huyo kuboreka na klabu yake ya sasa.
    Inafahamika kwamba Roberto Mancini anataka kumsajili tena mchezaji huyo aliyekuzwa Man City na kuna imani ataendelea vizuri kisoka akiwa Etihad.
    Sturridge amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake Chelsea na anaangalia upya mustakabali wake baada ya kuwa anasugua makalio benchi miezi ya mwishoni mwa msimu, kiasi cha kukosa nafasi kwenye kikosi cha England cha Euro 2012.
    City inapewa nafasi kubwa ya kuinasa saini ya kinda huyo wa miaka 22, anahusishwa mno na mpango wa kurejea Manchester na alipigwa picha hivi karibuni katika mapumziko, akiwa na Micah Richards, visiwa vya Caribbean.
    Anaangalia mustakabali wake katika wakati ambao Chelsea inakisuka upya kikosi chake katika safu ya ushambuliaji, kwa kubeba  nyota wapya kama Hulk, Eden Hazard na Marko Marin, wakati Kevin De Bruyne pia atatua moja kwa moja Stamford Bridge kwa ajili ya msimu ujao.
    Chelsea itataka pauni Milioni 12 kumuachia Sturridge, ambaye aliwekwa kama mchezaji wa ‘spea’ kwenye kikosi cha England, kufutaia msimu ambao aliifungia klabu yake mabao 13 na kuichezea mechi mbili timu yake ya taifa.
    Pamoja na hayo, City ilikubaliana na Chelsea kupata asilimia 15 iwapo nyota huyo atauzwa wakati inamuuza mchezaji wake huyo wa zamani wa akademi yao, kwenda Stamford Bridge mwaka 2009 na kwa sababu hiyo ina matumaini ya kumsajili kwa pauni Milioni 10 tu.
    Vyanzo vimesema kwamba kinda huyo wa miaka 22, mshahara wa pauni 65,000 kwa wiki anazopewa na Chelsea mchezaji huyo haliwezi kuwa tatizo kwa City.
    Mancini anamzimikia kinoma Sturridge na aliwahi kusema siku chache baada ya kuanza kazi Etihad kwamba anasikitika kijana huyo kuuzwa Chelsea.
    Sturridge amechanganyikiwa na hafurahii kupangwa pembeni badala ya nafasi ya mshambuliaji wa kati, jambo ambalo limemponza hadi kupoteza namba yake katika kikosi cha England.
    Baada ya kiwango chake kushuka, akawa anakaa benchi bila kutumika kabisa katika fainali zote, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY KUMSAJILI STURRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top