Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya

MANCHESTER UTD WATAKA KUSAJILI BEKI WA BARCELONA

KOCHA Brendan Rodgers, ambaye anatarajiwa kutambulishwa rasmi leo kuwa kocha wa Liverpool, anaweza kuondoka na wachezaji wake watatu wa zamani: Scott Sinclair, mwenye umri wa miaka 23, Gylfi Sigurdsson, miaka 22, na Ashley Williams, miaka 27.
KIUNGO wa Swansea, Joe Allen, mwenye umri wa miaka 22, pia ameorodheshwa katika orodha ya wachezaji wanaokwenda Anfield - ingawa kinda huyo bado mkataba wa miaka mitatu na katika klabu yake hiyo ya Wales na anaweza kuigharimu Liverpool pauni Milioni 10.
KLABU ya Manchester United imejiunga katika mbio za kuinasa saini ya kiungo wa Valencia, Jordi Alba, mwenye umri wa miaka 23. Beki huyo wa kushoto pia anawaniwa na Barcelona.
Bayer Leverkusen rule out buying Dimitar Berbatov
KLABU ya Bayer Leverkusen imeghairi mpango wa kumchukua Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka  31, labda klabu yake ya sasa, Manchester United imtoe bure mshambuliaji wake huyo.
KLABU ya Manchester City inajiandaa kuwapiga bao wapinzani wao wa Jiji, Man United katika kumsajili kiungo Mholanzi,  Wesley Sneijder, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Inter Milan.
MSHAMBULIAJI wa Norwich, Grant Holt, mwenye umri wa miaka 31, anajiandaa kumfuata kocha wake, Paul Lambert katika klabu ya Aston Villa aliyohamia.

MOURINHO AMFAGILIA RODGERS

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amemwagia ujiko kocha mwenzake wa zamani Chelsea, Brendan Rodgers kwamba atarejesha enzi za furaha katika klabu ya Liverpool.
MWENYEKITI wa Wigan, Dave Whelan anaamini Aston Villa si klabu tosha kwa Roberto Martinez.
KOCHA wa klabu ya Tottenham, Harry Redknapp atataka kujua kama bado anaungwa mkono na bodi ya klabu hiyo, kabla ya kuamua kufuata ofa ya kwenda kufundisha  soka Qatar anakotakiwa kwa maslahi mazuri.
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas alilipwa fidia ya pauni ya Milioni 12 alipofukuzwa katika klabu hiyo, Machi mwaka huu.
Celtic boss Neil Lennon a target for Norwich
KLABU ya Norwich iko tayari kumchukua kocha wa Celtic, Neil Lennon akazibe pengo la Paul Lambert, anayejiandaa kutua Aston Villa.

CHELSEA WAJIANDAA NA ZIARA YA MAREKANI

NYOTA wa klabu ya Chelsea, wameanza kujiandaa kwa ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.