• HABARI MPYA

    Tuesday, April 17, 2012

    REAL YABISHA HODI FAINALI ULAYA

    Ozil katikati ya msitu
    Ozil akishangilia bao muhimu
    USHINDI wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid utatosha kwa Real Madrid kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
    Hiyo inafuatia kufungwa mabao 2-1 usiku huu kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa na wenyeji Bayern Munich.
    Katika mchezo huo, Bayern ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17, mfungaji Frank Ribery kabla ya Ozil kuisawazishia Real dakika ya 53.
    Mario Gomez ndiye aliyeifungia Munich bao la ushindi ‘usio na raha’ dakika ya 90 usiku huu.
    Kocha Jose Mourinho alikasirika baada ya bao hilo kuingia kwa sababu alitarajia sare ya 1-1, lakini baada ya mechi alikuwa mwenye tabasamu pana.
    Kesho, Uwanja wa Stamford Bridge Chelsea watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi, Barcelona katika Nusu Fainali nyingine ya kwanza ya michuano hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL YABISHA HODI FAINALI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top