![]() |
| Tibaigana, Mwenyekiti Kamati ya Rufaa |
KIKAO cha cha Kamati ya Nidhamu
ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, kilichokuwa kifanyike kesho, kujadili
rufani ya Yanga kupinga kunyang’anywa pointi tatu kwa kumchezesha Nadir Haroub ‘Cannavaro’
katika mechi dhidi ya Coastal Union, kimeahirishwa.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti
wake Kamanda Mstaafu wa Polisi, Kanda Maalum Dar es Salaam, Alfred Tibaigana
sasa kitafanyika Jumanne ijayo, (Aprili 17 mwaka huu) saa 9 alasiri kwenye
ofisi za TFF.
Wakati huo huo: Vyama vya mpira
wa miguu vya mikoa 17 ya Tanzania Bara vimewasilisha majina ya mabingwa wake
kwa ajili ya Ligi ya Taifa iliyopangwa kuanza Aprili 22 mwaka huu katika vituo
vitatu.
Mikoa hiyo na mabingwa wake
katika mabano ni Kigoma (Kanembwa FC ya Kibondo), Kilimanjaro (Forest FC ya
Siha), Ruvuma (Mighty Elephant ya Songea), Dodoma (CDA), Rukwa, (Mpanda Star ya
Mpanda), Iringa (Kurugenzi FC ya Mufindi) na Lindi (Lindi SC).
Mingine ni Mtwara (Ndanda FC),
Shinyanga (Mwadui FC), Mara (Polisi Mara), Singida (Aston Villa), Arusha
(Flamingo SC) na Tabora (Majimaji FC). Mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa
wake ni Manyara, Dar es Salaam, Mwanza, Tanga, Morogoro, Pwani na Kagera.



.png)
0 comments:
Post a Comment