![]() |
| El Classico la Ghana inakuwaga hivi |
WAPINZANI wa jadi katika soka ya
Ghana, Asante Kotoko na Hearts of Oak watamenyana Jumapili katika Ligi Kuu ya
nchini humo, Uwanja wa Baba Yara, Kumasi.
Ikijukana kwa jina la ‘El-Classico
ya Ghana,’ barabara zote zitaelekea Kumasi; maarufu kama Jiji la Bustani kwa
watu wa matawi ya juu.
Mechi baina ya timu hizo mbili
inavutia mno na wapenzi wa soka na huwa kivutio kikubwa inapowadia na
wafanyabiashara hunufaika kiuchumi kwa kuuza bidhaa zao uwanajni.
Kama ilivyo ada Uwanja wa Baba
Yara, unatarajiwa kupambwa na rangi nyekundu za Asante Kotoko na njano zenye bluu na nyekundu kidogo za
Hearts of Oak.
Timu ya Porcupine Warriors inawazidi
vigogo hao pointi 10 katika msimamo wa Ligi Kuu.
Kwa kuzingatia kwamba Hearts of
Oak imeshinda mechi tatu zilizopita dhidi ya wapinzani wao hao katika Uwanja
huo huo, wenyeji watakuwa chini ya shinikizo hasa ikizingatiwa pia wanawania
taji la kwanza la Ligi Kuu tangu 2008.
Kivutio zaidi ni katika mabenchi
ya klabu zote, wote wana makocha ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya
Ghana, Black Stars.
Maxwell Konadu yupo klabu yake
ya zamani, Asante Kotoko wakati Nahodha wa zamani wa timu ya taifa, Charles
Akonnor yuko Hearts of Oak.
Akonnor ameiongoza Hearts of Oak
kushinda mechi zao mbili kati ya tatu zilizopita tangu aanze kazi, lakini
amesema mchezo huo umekuja katika wakati mbaya.
Katika mechi 46 ambazo Asante
Kotoko walikuwa wenyeji; wameshinda 16, Hearts of Oak 18 na 12 ziliisha kwa
sare.
Katika mechi nyingine,
Ashantigold itasafiri Port City kumenyana na Tema Youth wakati Medeama SC na
Bechem United watamenyana Uwanja wa Tarkwa Park.
Nayo timu ya zamani ya kipa wa
Yanga, Yaw Berko, Liberty Professionals itaonyeshana kazi na Hearts of Lions,
Aduana Stars na Berekum Arsenals na Dwarfs dhidi ya Wassaman.
Mabingwa watetezi, Berekum
Chelsea wagtacheza na Edubiase FC kwenye Uwanja wa Golden City Park.



.png)
0 comments:
Post a Comment