![]() |
| Terry kushoto, Lampard kulia na Kalou katikati, leo watapona kwa Barca? |
![]() |
| Messi akifunga dhidi ya AC Milan katika Robo Fainali, leo atavunja mwiko wake wa kutoifunga Chelsea? |
KUNA tatizo kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea huku David Luiz
akitarajiwa kukosekana kwenye mechi ya leo dhidi ya Barcelona baada ya kutolewa
Uwanja wa Wembley dhidi ya Tottenham Jumapili.
Mbali na kisiki hicho, Gary Cahill naye pia anasumbuliwa na
maumivu ya mguu. John Terry ataendelea kucheza licha ya kwamba naye ni majeruhi
na Branislav Ivanovic anaweza kuchukua nafasi ya Jose Bosingwa katika beki ya
kulia, ambaye anatumikia adhabu aliyopewa katika Nusu Fainali ya Kombe la FA.Pamoja na hayo, Kocha Roberto Di Matteo lazima aamue kujenga imani juu ya wachezaji waliompa ushindi wa 5-1 dhidi ya Spurs.
Dider Drogba na Frank Lampard wote walifunga Jumapili, hivyo wana nafasi kubwa ya kuanza pamoja leo, ingawa Fernando Torres, ambaye alianza katika mechi zote dhidi ya Benfica, atakuwa na matumaini ya kuanza kwenye 11 wa kwanza.
Barcelona haina majeruhi wapya na zaidi inafurahia kupona na kurejea kazini kwa wachezaji wake Dani Alves, Gerard Pique, Seydou Keita na Ibrahim Afellay. Lakini hatari moja tu kwao ni kwamba Javier Mascherano na Carles Puyol wana kadi moja moja za njano wote.
JE WAJUA?
•Chelsea ilikutana mara ya mwisho na Barcelona Mei mwaka 2009, kwenye michuano kama hii na hatua kama hii. Baada ya sare ya bila kufungana kwenye mechi ya kwanza, Barca walifuzu kuingia fainali kwa bao la dakika ya mwisho la Andres Iniesta, ambalo lilikuwa la kusawazisha baada ya Michael Essien kutangulia kufunga. Barca ilifuzu kwa faida ya bao la ugenini.
•The Blues wana rekodi nzuri wakicheza nyumbani msimu huu
katika Ligi ya Mabingwa. Vijana wa Di Matteo wamecheza mechi tano, wameshinda
tano, wamefunga mabao 16 na wamefungwa mawili tu.
•Hii ni mara ya sita kwa timu ya London kucheza Nusu Fainali
ya Ligi ya Mabingwa ndani ya miaka tisa.
Lakini wameshinda mechi moja tu, walipoifunga kwa jumla ya
mabao 4-3 mwaka 2008.
•Timu ya Stamford Bridge haijawahi kutwaa Kombe lolote la
Ulaya, zaidi ya kushika nafasi ya pili mwaka 2008.
•Barcelona ilipokwenda mara ya mwisho London, Mei mwaka jana
kwenye Uwanja wa Wembley, iliifungta Manchester United mabao 3-1 na kutwaa taji
la nne la Ligi ya Mabingwa.
•Kama mabingwa hao watetezi watatwaa taji hilo msimu huu,
itakuwa mara ya nne ndani ya miaka saba na itakuwa timu ya kwanza kutetea taji tangu
AC Milan mwaka 1990.
•Huu ni msimu wan ne mfululizo, Barcelona inacheza Nusu
Fainali Ligi ya Mabingwa. Timu ya mwisho kuifunga Barca katika hatua hii,
ilikuwa ni Inter Milan mwaka 2010.
•Lionel Messi amekutana
na Chelsea mara sita katika Ligi ya
Mabingwa, lakini hajawahi kutikisa nyavu za The Blues.
•Wakati timu hizo zilipokutana katika Robo Fainali mwaka
2000, Barcelona iliifunga Chelsea 5-1 katika mechi ya marudiano Uwanja wa Camp
Nou.
Katika mechi hiyo, Roberto Di Matteo alicheza kwenye kikosi
cha kwanza cha The Blues, wakati Pep Guardiola alichezea Barca- leo wote
wanakaa kwenye mabenchi ya timu zao. Itakuwaje? Hili si game la kukosa.
VIKOSI VYA LEO:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Mikel, Lampard,
Ramires, Mata, Kalou na Drogba.
BARCELONA: Valdes, Puyol, Mascherano, Pique, Alves, Xavi,
Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi na Pedro.




.png)
0 comments:
Post a Comment