• HABARI MPYA

    Thursday, April 19, 2012

    GUARDIOLA AWAPA NAFASI CHELSEA, AHOFIA WATAPAKI TENA BASI CAMP NOU

    Drogba baada ya kutupia mpira kwenye nyavu
    KOCHA wa Barcelona, Pep Guardiola amesema kwamba Chelsea wana nafasi kubwa ya kuingia Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, kufuatia ushindi wao wa 1-0 jana kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
    Beo pekee la Didier Drogba sekunde chache kabla ya mapumzi, liliipa ushindi huo timu hiyo ya Magharibi mwa London kabla ya mechi ya marudiano wiki ijayo Camp Nou.
    "Chelsea wana nafasi sasa, lakini tuna dakika 90 mbele na lazima tujaribu kufanya vizuri ili tufuzu," alisema Guardiola katika taarifa iliyoifikia bongostaz.blogspot.com.
    "Lengo letu ni kutengeneza nafasi 24 kama tulivyofanya leo (jana) na kugunga bao. Lazima tujitoe muhanga zaidi, lakini nimewaambia wachezaji wangu kwamba tulitengeneza nafasi leo (jana), kasha tutafanya hivyo na Camp Nou pia.
    "Tunatambua kwamba ili kufunga bao lazima tutengeneze nafasi nyingi. "
    Barcelona ilitawala mchezo huo ndani ya dakika zote 90, lakini ilishindwa kuziona nyavu za Blues.
    Guardiola amesema timu yake haikuwa na bahati mbele ya lango na anaamini kwamba Chelsea watacheza kwa kujihami kwenye mchezo wa marudiano.
    "Matokeo ndiyo haya," alisema. "Dhahiri tulipata nafasi nyingi katika mchezo wa ugenini wa Nusu Fainali, lakini tunajua kutofunga ugenini itakuathiri.
    "Wamefunga bao na fikiria, kitu kile kile kitatokea Camp Nou, wachezaji 10 wa Chelsea kupaki kontena kwenye eneo lao.
    "Hii ni nzuri kwetu, tutakomaa nayo na kama tunataka kuitwa timu bora, tunatakiwa kushinda.
    Pamoja na hayo, kocha huyo wa timu hiyo ya Catalan, hakutaka kuponda mbinu za Roberto Di Matteo, akisema. "Mimi si wa kusema wamechezaje.
    "Ni wao wenyewe wanaotakiwa kujua wanapaswa kuchezaje, lakini hatuwezi kusahau ukweli kwamba wamefika Nusu Fainali ya Ligi Mabingwa mara sita katika miaka tisa iliyopita.
    "Matokeo si halali? Hapana, hii ni soka. Haushindi kwa kumiliki sana mpira; kama ingekuwa hivyo tungekuwa tunashinda kila wakati.
    "Unatakiwa kufunga mabao na hicho ndicho tutakachojaribu kufanya kwenye mechi ya marudiano."
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GUARDIOLA AWAPA NAFASI CHELSEA, AHOFIA WATAPAKI TENA BASI CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top