• HABARI MPYA

    Thursday, June 21, 2012

    DIAMOND KUTINGA NA MKOKO WAKE MPYA MISS DAR INTER COLLEGE


    Diamond akiwa na gari lake jipya. Picha na Teen TZ

    Na Princess Asia
    MFALME wa Bongo Fleva, Nassib Abdul au Diamond Platinum, kesho atatinga na mkoko wake mpya wa ‘bei chafu’ alioununua hivi karibuni katika shindano la Miss Dar Inter College 2012 itakayofanytika kwenye ukumbi wa Makumbusho, katikati ya Jiji karibu kabisa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
    Mtu mmoja wa karibu wa Diamond, ameaimbia BIN ZUBEIRY kwamba Diamond atatinga na mkoko huo katika shoo hiyo, ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwenda nayo kazini tangu itue nchini.
    “Mshikaji atakuja na mkoko wake mpya, nah ii itakuwa ni mara ya kwanza kabisa tangu mzigo huo utue nchini,”alisema mtu huyo wa karibu wa Diamond, msanii aliye juu ‘kinoma’ hivi sasa bongo.
    Jana walimbwende wa Miss Dar Inter College walijivinjari katika ukumbi wa Billicanas kwenye shoo ya Usiku wa wa Mwafrika iliyopambwa na bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.
    Shindano hilo, litakaloshirikisha mabinti wenye upeo wa hali ya juu kutokana na ukweli kwamba wanatoka vyuoni, mbali na burudani ya Mfalme wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, pia litapambwa na burudani ya bendi mpya ya muziki wa dansi inayokuja juu hivi sasa, Skylight.
    Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail Mkingiye ‘Dodo’, ameiambia BIN ZUBEIRY maandalizi kwa ujumla yanaendelea vizuri na warembo 14 watakaoshiriki shindano hilo leo watafanyiwa usaili Dar es Salaam
    “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Inter College anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania,” alisema.
    Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati taji la Miss Inter College linashikiliwa na binti kutoka IFM, Rose Msuya.
    Warembo wawili wa Inter College walishiriki fainali za Miss Tanzania mwaka jana na kufanya vizuri, mbali na Rose mwingine ni mshindi wake wa pili, Blessing Ngowi.
    Dina aliyewahi kuandikia pia magazeti ya Majira, Spoti Starehe na kutangazia Radio Times, aliwataja warembo wanaoshiriki shindano hilo kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacqueline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
    Amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Redd’s Premium, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Clouds Media Group blog za Michuzi, Dina Ismail, BIN ZUBEIRY, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIAMOND KUTINGA NA MKOKO WAKE MPYA MISS DAR INTER COLLEGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top