MIAKA mine iliyopita, Andres Iniesta alifunga bao pekee la ushindi Hispania ikitwaa ubingwa wa Dunia kwa kuifunga Uholanzi 1-0 katika fainali ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.
Lakini kipa Iker Casillas alikuwa shujaa wa mechi kwa kuokoa michomo mingi ya hatari, ukiwemo wa aliobaki ana kwa ana na Arjen Robben ambaye hakuamini macho yake.
Jana, Hispania ikifungwa 5-1 na Uholanzi katika mchezo wa Kundi B Kombe la Dunia, Casillas alikuwa kama 'shati' langoni kwa kutunguliwa kwa urahisi mno.
Alifungwa kwa kichwa cha umbali wa yadi 51 na Robin van Persie- akafungwa tena kwa kulambwa chenga na mshambuliaji huyo wa Manchester United. Akafungwa kwa shuti la mpira wa adhabu na Wesley Sneidjer. Ovyo kabisa. Naam, bila shaka sasa umewadia mwisho wake na kuna uwezekano kocha Vicente del Bosque kuanza kumtumia kipa wa Manchester United, David Gea..
Wa kujifunzia kufunga: kipa Iker Casillas amekwisha na sasa bora arudi benchi kabla ya kustaafu
Kichwa kinauma: Casillas anampa wakati mgumu kocha Vicente del Bosque wa kuamua juu ya kipa mamba moja wa timu hiyo kwa sasa
Zamu yake: David de Gea kushoto bila shaka sasa ni wakati wake kukabidhiwa lango la Hispania
0 comments:
Post a Comment